KIKOSI cha Yanga kinachonolewa na Kocha Mkuu, Nasredine Nabi kimekwama kuvuna pointi tatu mbele ya Tanzania Prisons kwenye mchezo wa ligi uliochezwa Uwanja wa Mkapa.
Baada ya dakika 90 kukamilika Mei 9,hakuna timu ambayo iliweza kucheka na nyavu kwenye mchezo huo uliokuwa na kasi kubwa.
Mshambuliaji wa Yanga, Fiston Mayele katika mchezo huo alikosa penalti baada ya kupaisha na kufanya ashindwe kufikisha bao la 13 ndani ya ligi.
Ilikuwa ni dakika ya 38 kwenye kipindi cha kwanza nyota huyo aliweza kukosa penalti iliyosababishwa na Feisal Salum.
Anabakiwa na mabao yake 12 akiwa sawa na George Mpole wa Geita Gold ambaye huyu ni mzawa.
Yanga inabaki kuwa namba moja kwenye msimamo ikiwaacha wapinzani wao Simba kwa pointi 11 kwa kuwa wao wana pointi 57 baada ya kucheza mechi 23 huku Simba wakiwa na pointi 46 baada ya kucheza mechi 22.

No comments:
Post a Comment