KIKOSI cha Simba kimeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Kagera Sugar kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Mkapa.
Ilikuwa ni moja ya mchezo mzuri leo Mei 11 kwa mashabiki ambao walijitokeza kushuhudia burudani ya ligi kutokana na timu zote kucheza mpira wa pasi bila nguvu nyingi.
Mabao ya Kibu Dennis na John Bocco yalitosha kuipa pointi tatu Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Pablo Franco.
Huu unakuwa ni ushindi wa pili mfululizo kwa Simba Uwanja wa Mkapa baada ya mchezo uliopita kushinda mabao 4-1 dhidi ya Ruvu Shooting.
Ushindi huu unaifanya Simba kufikisha pointi 49 na wamecheza mechi 23 huku Kagera Sugar ikiwa nafasi ya 7 kwenye msimamo na pointi 29.

No comments:
Post a Comment