SIMBA YAIVUTIA KASI MBEYA CITY - Dizo Click

Dizo Click

Hot

Post Top Ad

Tuesday, 22 November 2022

SIMBA YAIVUTIA KASI MBEYA CITY

 


JUMA Mgunda, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa wapo tayari kwa mchezo wa kesho dhidi ya Mbeya City.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Sokoine ukiwa ni wa ligi.

Simba imetoka kupata ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Ruvu Shooting kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkapa huku Mbeya City wakigawana pointi mojamoja na Geita Gold.

Mgunda amesema:"Utakuwa ni mchezo mgumu na kila mmoja anatambua kwamba kazi ni ngumu kwani wapinzani wetu wapo vizuri.

"Tutajitahidi kutafuta ushindi na wachezaji wapo tayari kwa ajili ya mchezo huo na tutapambana kwa ajili ya kupata ushindi,".

Ni Bocco alifunga hat trick kwenye mchezo uliopita na bao moja mali ya Shomari Kapombe.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad