YANGA WASEPA NA POINTI TATU ZA DODOMA JIJI - Dizo Click

Dizo Click

Hot

Post Top Ad

Tuesday, 22 November 2022

YANGA WASEPA NA POINTI TATU ZA DODOMA JIJI

 


DAKIKA 90 zimekamilika kwa Yanga kusepa na pointi tatu ugenini leo mchezo wa ligi.


Ubao wa Uwaja wa Liti umesoma Dodoma Jiji 0-2 Yanga na mabao yote yakifungwa na mshambuliaji Fiston Mayele.

Ni Mayele alianza kupachika bao la kuongoza kipindi cha kwanza dakika ya 41 akiwa ndani ya 18 na kuwafanya Dodoma Jiji kuwa nyuma kwa bao moja.

Kipindi cha pili tena yuleyule Mayele aliwatungua bao la pili Dodoma Jiji dakika ya 67 na kuwapoteza mazima wapinzani hao.

Sasa Mayele anakuwa namba moja kwa utupiaji akiwa na mabao 8 kibindoni ndani ya ligi msimu huu.

Pia Yanga inarejea kwenye namba moja ikiwa na pointi 29 ikiwa sawa na Azam FC tofauti ya mabao ya kufunga na kufungana.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad