CROATIA USO KWA USO NA BRAZIL KOMBE LA DUNIA - Dizo Click

Dizo Click

Hot

Post Top Ad

Tuesday 6 December 2022

CROATIA USO KWA USO NA BRAZIL KOMBE LA DUNIA


DOMINIK Livakovic kipa wa Croatia ameibuka kuwa shujaa wakati timu yake ya taifa ikitinga hatua ya robo fainali kwa ushindi wa penalti 3-1 dhidi ya Japan baada ya kuokoa penalti tatu kwenye mchezo uliokuwa na ushindani mkubwa hatua ya 16 bora, Kombe la Dunia 2022,Qatar.

Mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Al Janoob ni mashabiki 42,523 walishuhudia mabao ya timu zote mbili yakifungwa kwenye kila kipindi kimoja ambapo ni Daizen Maeda alifunga bao la kuongoza kwa Japan dakika ya 43 na Ivan Perisic huyu alipachika bao dakika ya 55 kwa pigo la kichwa chenye ujazo.

Kutokana na sare hiyo ngoma ilipelekewa kuongezwa dakika 30 ambapo bado ngoma ilikuwa nzito kwa timu zote ubao ukasoma 1-1 na kupekelekea mshindi kusakwa kwa mikwaju ya penalti hapo ndipo shujaa Livakovic akaibuka.

Livakovic kipa wa Croatia anakuwa ni kipa wa tatu kwenye Kombe la Dunia kuokoa penalti tatu kwenye mchezo mmoja na wengine ambao waliwahi kufanya hivyo ni kipa wa Ureno Ricardo mwaka 2006 ilikuwa dhidi ya England na kipa wa Croatia, Danijel Subasic ilikuwa kwenye mchezo dhidi ya Denmark 2018.

Huu unakuwa ni mchezo wa kwanza kwenye Kombe la Dunia 2022 Qatar kufika kwenye muda wa nyongeza kwa kuwa timu zote zilikuwa zinamalizana ndani ya dakika 90.

Ushindi huo unaifanya timu ya Croatia kusaka ushindi kwenye mchezo wa hatua ya robo fainali dhidi ya Brazil unaotarajiwa kuchezwa Desemba 9.

Kipa wa Croatia alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mchezo huo ambapo baada ya mchezo Kocha Mkuu wa timu hiyo ambayo imetinga hatua ya robo fainali ameweka wazi kuwa ni moja ya kipa mzuri.

"Tumekuwa na kipa mwenye maajabu mengi na uwezo mkubwa, ameokoa kila hatari ambayo ilikuwa inatukabiri na ameokoa penalti kwa uimara mkubwa,".




No comments:

Post a Comment

Post Top Ad