KIPA WA MPIRA MIKONO 100 - Dizo Click

Dizo Click

Hot

Post Top Ad

Tuesday 6 December 2022

KIPA WA MPIRA MIKONO 100


 WEKA kando kutunguliwa bao moja mbele ya Yanga kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkapa, bado uimara wa kipa aliyeanza ulikuwa kwenye kiwango.


Desemba 4, wakati ubao wa Uwanja wa Mkapa ukisoma Yanga 1-0 Tanzania Prisons,mchezaji bora kwa upande wangu alikuwa ni kipa Hussein Abel.


Jitihada zake ndani ya dakika 89 zilikuwa kubwa mwanzo mwisho akikamilisha majukumu yake kuzuia mpira usizame kwenye nyavu zake.


Safu yake ya ulinzi ilikuwa na Jumanne Elifadhili ambaye aliokoa hatari dakika ya 36 na pia Yusuph Mlipili yeye aliokoa hatari dakika ya 2,27 kazi ilikuwa kubwa kwelikweli.


Kuna nyakati msako wa Yanga ulikuwa ni wa juu huku wakimtumia nyota wao Feisal Salum kuachia mashuti ya mbali bado kijana alikuwa imara.


Moja ya mashuti ambayo Feisal alilenga lango ilikuwa ni dakika ya 41 na 60 haya yote yaligotea kwenye mikono ya Abel.


Ana kazi kubwa ya kuzidi kupambana kubaki kwenye ubora na kupewa nafasi ya kucheza mechi atakazopata na asiwe mchezaji wa mchezo mmoja.


Huwa inatokea wachezaji wanafanya vizuri mchezo mmoja lakini wanashindwa kuwa na mwendelezo kwenye mechi nyingine.


Kazi bado inaendelea wanasema kuvunjika kwa koleo sio mwisho wa uhunzi.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad