DADA wa nyota wa Timu ya Taifa ya Ureno, Cristiano Ronaldo amelalamika kuwa kaka yake alinyanyaswa baada ya kupewa nafasi ya kuanzia benchi kwenye mchezo wa hatua ya 16 bora Kombe la Dunia Qatar 2022 dhidi ya Uswisi mchezo uliochezwa Desemba 6,2022.
Elma Aveiro ambaye ni dada wa nyota huyo ameweka wazi kuwa anaamini wakati unakuja na yote anayofanyiwa yatapata majibu.
Mshambuliaji wa Benfica, Goncalo Ramos alianza kwenye nafasi ya ushambuliaji badala ya Ronaldo na alifunga hat trick kwenye mchezo huo wakati Ureno ikishinda kwa mabao 6-1 dhidi ya Uswisi.
Ronaldo kwenye mchezo huo alipata nafasi ya kucheza kwenye mchezo huo kipindi cha pili ikumbukwe kwamba ni mshindi mara tano wa tuzo ya Ballon d’Or na hana uhakika kama anaweza kuanza kwenye kikosi cha kwanza kwenye mchezo wa hatua ya robo fainali Kombe la Dunia dhidi ya Morocco kutoka Afrika Jumapili.
Nyota huyo mwenye miaka 37 ni moja ya mastaa ambao wanafuatiliwa na wengi na kwa sasa hana timu baada ya Manchester United kufikia makubaliano ya kuvunja mkataba wake.
Baada ya maamuzi ya Ronaldo kuwekwa kando kwenye kikosi cha kwanza dadaye Elma Aveiro aliandika kwenye ukurasa wake wa Instagram kuwa: Sijui kwa nini na sijui kwa nini sielewi kuhusu hili lakini nina amini kwama kuna majibu mazuri kuhusu haya na tutajibiwa na Mungu baadaye bado hajafeli tusubiri na tuone.
Aveiro baadaye aliendelea baada ya timu ya Ureno kushinda na alipoulizwa kutoa maoni yake na Mwandishi wa Habari wa CNN: "Ndio najua Ronaldo hajafika mwisho, ndiyo, Ronaldo hatacheza milele, bahati mbaya sana hakufunga bao kwa sasa umri umekuwa mkubwa Ureno inaonekana kwamba haimuhitaji Ronaldo.
‘Tumezungumza kuhusu kile ambaco tumekisikia lakini yote kwa yote hayo sio muhimu yale yote ambayo amefanya nadhani wameanza kusahau sasa wanahitaji aombe msahamaha na hawamuhitaji yeye nitalikumbuka hili na nitalizungumzia baadaye.
‘Ni aibu kumdhalilisha mwanaume ambaye amejitoa kwelikweli, lakini baadaye tutaona zaidi ya haya,".

No comments:
Post a Comment