GHANA BANA WALIZUNGUA - Dizo Click

Dizo Click

Hot

Post Top Ad

Saturday, 3 December 2022

GHANA BANA WALIZUNGUA


 TIMU ya taifa ya Ghana kwenye Kombe la Dunia tangu mwaka 1966 wakati rekodi zinatajwa kuanza kukusanywa inakuwa timu ya kwanza kukosa penalti mara mbili kwa timu moja.


Ilikuwa ni mwaka 2010 na 2022 mbele ya timu ya taifa ya Uruguay jambo ambalo linawapasua kichwa kwa sasa kuweza kutatua wakati ujao.


Wakati wakifungwa mabao 2-0 dhidi ya Uruguay kwenye mchezo wa makundi Desemba 2,2022 ni staa wao Andre Ayew alikosa penalti ambaye ni nahodha.

Licha ya kufungwa na Uruguay kushinda wote wameondolewa kwenye michuano ya Kombe la Dunia 2022 Qatar kutoka kundi H baada ya Korea Kusini kufanya maajabu na kushinda mchezo wao dhidi ya Ureno.

Korea Kusini iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 baada ya kupindua meza mbele ya timu hiyo yenye Cristiano Ronaldo.

Kwenye mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Al Janoub mbele ya mashabiki 43,443 staa wa Uruguay, Luis Suarez hakuwa na chaguo zaidi ya kumwaga machozi licha ya ushindi ambao walipata.

Mabao ya staa wao Giorgian de Arrascaeta ambaye alikuwa nyota wa mchezo alifunga dakika ya 26 na 32 hayakutosha kuipeleka timu hiyo hatua ya 16 bora nao watarejea nyumbani kama Waafrika Ghana ambao walipoteza mchezo huo.

Kilichowatibulia Uruguay ni ushindi ambao walipata timu ya taifa ya Korea Kusini wa mabao 2-1 dhidi ya Ureno kwenye mchezo wa makundi jambo lililowafanya wawe tofauti kwenye mabao ya kufunga na kufungwa.

Ambapo Uruguay kibindoni wana mabao mawili huku Korea Kusini wakiwa na mabao manne hivyo hatua ya 16 bora Desemba 5 itakuwa kati ya Brazil dhidi ya Korea Kusini na Ureno dhidi ya Switzerland.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad