HAWA HAPA WAMOROCCO MIKONONI MWA SIMBA CAF - Dizo Click

Dizo Click

Hot

Post Top Ad

Monday, 12 December 2022

HAWA HAPA WAMOROCCO MIKONONI MWA SIMBA CAF


 KLABU ya Simba ya Tanzania, imepangwa katika kundi C katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika.

Kwenye kundi hilo ambalo ikiwa Simba watapanga kete vizuri wanaweza kutusua na wakibugi watapotezwa itakutana na Vipers kutoka Uganda, Horoya ya Guinea na Raja Cassablanca ya Morocco.

Simba ilifanikiwa kuingia katika Hatua ya Makundi katika mashindano ya Klabu Bingwa na sasa itakuwa na kazi ya kupambana na miamba hiyo, ili kusonga mbele.

Kazi kubwa kwa wawakilishi hao ni kusaka pointi tatu kwenye mechi ambazo watacheza jambo litakalowapa tiketi ya kusonga mbele.

Chini ya Kocha Mkuu, Juma Mgunda timu hiyo ilifanikiwa kutinga hatua ya makundi jambo ambalo lilikuwa kwenye mipango ya Simba.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad