NAHODHA wa Timu ya Taifa ya Ureno, Cristiano Ronaldo amebainisha kuwa hataachana na timu hiyo kwa sasa licha ya kutoka uwanjani akimwaga machozi baada ya timu hiyo kuondolewa kwenye hatua ya nusu fainali ya Kombe la Dunia 2022, Qatar.
Timu hiyo ambayo ilikuwa inapewa nafasi ya kupata ushindi kwenye mchezo huo haikuamini macho yake baada ya kutunguliwa bao 1-0 dhidi ya Morocco kwenye hatua hiyo ya robo fainali.
Ronaldo hakuwa na furaha kwa kuwa malengo yake ilikuwa ni kuona kwamba wanatinga hatua ya nusu fainali lakini ndoto hizo ziligonga mwamba kutoka kwa timu pekee kutoka Afrika iliyobaki kwenye Kombe la Dunia ambayo ni Morocco.
Bao la ushindi ambalo lilizamisha jahazi la Ureno lilifungwa na Youssef En-Nesyri dakika ya 42 ambalo lilitosha kuwapa ushindi Morocco waliokamilisha mchezo huo wakiwa pungufu baada ya nyota wao Walid Cheddira kuonyeshwa kadi nyekundu dakika ya 90+3
Nyota huyo mwenye miaka 37 jitihada zake naye ziligonga mwamba kwenye kuipa ushindi timu hiyo na sasa atakuwa miongoni mwa watazamaji wengine akiungana na Ghana, Qatar ambao ni wenyeji, Senegal ambazo zilifungashiwa virago.
Mreno huyo amebainisha kuwa ndoto zake kubwa ilikuwa ni kuona kwamba wanafanikiwa kutwaa taji la Kombe la Dunia lakini haijafanikiwa kwa kuwa wameondolewa katika hatua ya robo fainali.
Kwa sasa nyota huyo hana timu baada ya kufikia makubaliano ya kuachana na Manchester United kutokana na mahojiano aliyofanya hivi karibuni kuvujisha masuala ya timu huku akibainisha wazi kwamba hamheshimu Kocha Mkuu wa Manchester United Erik ten Hag.
Ujumbe wake ambao ameuacha unaonyesha kwamba bado ataendelea kutumikia Timu ya Taifa ya Ureno na hana mpango wa kustaafu kwa sasa hivyo huenda atakuwa miongoni mwa wale watakaoshiriki Kombe la Dunia lijalo.
"Kushinda Kombe la Dunia ilikuwa ni ndoto yangu kubwa na inaonekana kwamba ilikuwa ni ndoto yangu lakini haijafanikiwa kwenye maisha yangu ya mpira, bahati mbaya sana haijawa hivyo tumeshindwa kupata Kombe la Dunia ingekuwa ni jambo jema kwangu na timu ya Taifa pia kushinda,
"Mabao ambayo nimefunga kwenye Kombe la Dunia kwa uwepo wangu kwa zaidi ya miaka 16 pamoja na ushirikiano mkubwa ambao ninapata kutoka kwa wachezaji wenzangu bado kuna jambo ambalo nina amini walikuwa pamoja nasi, kweli tulijitoa kwa hali na mali," .
Morrocco ambayo imeifungashia virago Ureno inatarajiwa kumenyana na Argentina kwenye mchezo wa hatua ya nusu fainali Desemba 13,2022.

No comments:
Post a Comment