HII HAPA RATIBA YA LEO LIGI KUU BARA - Dizo Click

Dizo Click

Hot

Post Top Ad

Tuesday, 20 December 2022

HII HAPA RATIBA YA LEO LIGI KUU BARA

 


RUVU Shooting chini ya Kocha Mkuu, Mbwana Makata ina kibarua cha kusaka ushindi kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mtibwa Sugar.


Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Uhuru katika msako wa point tatu muhimu.


Mchezo uliopita Ruvu Shooting ilipoteza pointi tatu mbele ya Ihefu ambapo ilifungwa mabao 2-0 lile moja ni mali ya Obrey Chirwa na jingine Ruvu Shootin walijifunga kwenye harakati za kuokoa hatari.


Mbali na mchezo huo pia Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi itakabiliana na Coastal Union ya Tanga chini ya Joseph Lazaro.


Mchezo mwingine ni ule kati ya Namungo v Ihefu pale Uwanja wa Majaliwa.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad