MWISHO wa safari ya timu ya taifa ya Senegal kwenye Kombe la Dunia umegota mwisho baada ya kupoteza mchezo wa hatua ya 16 bora kwa kufungwa mabao 3-0 dhidi ya timu ya Taifa ya England.
Kwenye mchezo huo ambao wawakilishi kutoka Afrika bila ya uwepo wa nyota wao Sadio Mane walikubali kukamwa kufunga kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Al Bayt ambapo dakika ya 39 England walipachika bao a kwanza kupitia kwa Jordan Henderson ambaye alifunga bao la ufunguzi.
Bao hilo la Henderson linaingia kwenye rekodi ya washambuliaji wa England wenye miaka mingi kufunga kwenye Kombe la Dunia.
Nyota huyo amefunga bao hilo akiwa na miaka 32 na siku 170 ikiwa ni sawa na nyota Tommy Finney ambaye alifunga akiwa na miaka 36 na siku 64 mwaka 1958 ilikuwa dhidi ya USSR.
Inakuwa ni wakati bora kwa Kocha Mkuu wa England, Gareth Southgate kwa vijana wake kufanya vizuri kwenye mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa ndani ya uwanja na alishuhudia bao la pili likifungwa na Harry Kane dakika ya 45 ikiwa ni bao lake la kwanza kwenye mashindano ya Kombe la Dunia Qatar 2022.
Bukayo Saka alikamilisha kete ya tatu ilikuwa dakika ya 57 ya mchezo huo ulioshuhudiwa na mashabiki 65, 985.
Kocha huyo amesema kuwa vijana wake walicheza kwa kujiamini licha ya ushindani ambao walipata kwenye mchezo huo uliokuwa ni muhimu kwao kushinda.
"Vijana wamecheza kwa kujiamini na ninadhani hii inatokana nakuwa na uzoefu kwenye mechi ambazo tumecheza ni wakati mwingine wa kuendelea kuwa kwenye ubora katika mashindano haya,".
Sasa timu ya taifa ya England itakutana na mabingwa watetezi Ufaransa ambao walishinda mchezo wao wa hatua ya 16 bora kwa ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Poland.
Mchezo wao wa hatua ya robo fainali unatarajiwa kuchezwa Desemba 10,2022 nchini Qatar.

No comments:
Post a Comment