TIMU ya Taifa ya Croatia imewaengua Timu ya Taifa ya Brazil kwenye mchezo wa hatua ya robo fainali ya Kombe la Dunia na kutinga hatua ya nusu fainali.
Ushindi wa penalti 4-2 umewapa tiketi Croatia kuwafungashia virago timu pendwa Brazil iliyokuwa na staa wake Neymar ambaye hakuwa na namna ya kufanya na wala hakupiga penalti.
Ilikuwa ni kwenye mchezo uliochezwa usiku wa Desemba 9,2022 Uwanja wa Edacation City na ni mashabiki 43,893 walishuhudia mchezo wenye ushindani mkubwa ambapo ziliongezwa dakika 30 na kukamilisha dakika 120 kwenye sare ya kufungana bao 1-1.
Timu pendwa ya Brazil kwenye mashindano haya ya Kombe la Dunia Qatar 2022 ilikuwa inapewa nafasi kubwa ya kushinda mchezo huo mbele ya Croatia ambao walikuwa wanaonekana ni wepesi kufungika.
Lakini kwenye kipindi cha kwanza walikuwa wapo chini huku wakiwatumia nyota wao ikiwa ni pamoja na Luka Modric, Marcelo Brozovic na Mateo Kovacic kuwa kwenye mchezo na kuwazuia mastaa wa Brazil kwenye mpango kazi wao wa kusaka ushindi.
Licha ya kipindi cha pili timu ya Taifa ya Brazil kuimarika na kuongeza nguvu kwenye mechi hiyo ilikuwa ngumu kwao kuitungua ngome ya Croatia chini ya kipa Dominik Livakovic.
Neymar staa wa Brazil mara mbili alikosa nafasi ya kufunga wakati Livakovic akifanya kazi ya kuokoa hatari mara nyingi kwenye mchezo huo tena zile kubwa kutoka kwa Lucas Paqueta na Vinicius Jr.
Kwenye muda wa nyongeza Brazil wao waliendelea kutegeneza mashambulizi lakini Croatia waliendelea kuunda ukuta mgumu na kutengeneza nafasi chache za kufanya majaribio kwa mbali kuelekea kwenye lango lao na kushambulia kwa kushtukiza
Kwenye kipindi cha kwanza cha nyongeza Neymar alipachika bao la kuongoza dakika ya 105 lakini Croatia walirejea kwa kasi na kupata bao la kuweka usawa kupitia kwa Petkovic dakika ya 117 na lilikuwa ni shuti pekee ambalo lililenga lango kwa Croatia.
Brazil imeondolewa kwa mikwaju ya penalti ambapo Croatia wameshinda kwa penalti 4-2 na kuwafanya safari yao kugotea hapo huku Timu ya Taifa ya Croatia ikisubiri mshindi wa mchezo kati ya Argentina na Uswisi kucheza naye hatua ya nusu fainali.
Ni kwa mara ya pili kwenye Kombe la Dunia Croatia wanatinga hatua ya nusu fainali jambo ambalo lilikuwa halijatarajiwa.
Mastaa wa Brazili walikuwa wanasubiri kuandika rekodi ya kutinga hatua ya nusu fainali kisha fainali na kutwaa mara ya sita Kombe la Dunia ngoma imekuwa nzito.

No comments:
Post a Comment