AFCON IMEZIDI KUPAMBA MOTO, HAWA HAPA WANAKUTANA - Dizo Click

Dizo Click

Hot

Post Top Ad

Wednesday, 31 January 2024

AFCON IMEZIDI KUPAMBA MOTO, HAWA HAPA WANAKUTANA


KAZI inaendelea Ivory Coast kwenye msako wa bingwa mpya wa Kombe la Mataifa, Afrika, (AFCON) huku kila timu ikitamba kufanya vizuri.

Wababe wengi wamegotea kwenye hatua za makundi na wengine hatua ya 16 bora ikiwa ni pamoja na mabingwa watetezi Senegal yenye Sadio Mane ilipoondokewa kwa penalti 4-5 Ivory Coast baada ya kutoshana nguvu kwa kufungana bao 1-1 katika dakika 120.

Tanzania iligotea kwenye hatua za makundi ikiwa na pointi mbili baada ya kupata sare kwenye mechi mbili dhidi ya DR Congo yenye Henock Inonga anayecheza Klabu ya Simba na Fiston Maywele aliyewahi kucheza Yanga na Zambia ya Clatous Chama anayekipiga ndani ya kikosi cha Simba.

Wakati ulimwengu ukiipa nafasi Morocco kutinga hatua ya robo fainali dakika 90 zikaleta maajabu yake kwa timu hiyo iliyokuwa kundi F pamoja na Tanzania ikimaliza ikiwa nafasi ya kwanza safari yake imegota mwisho.

Hatua ya 16 bora imegota mwisho na hapa robo fanali Kombe la Mataifa Afrika, (AFCON) itakuwa namna hii kwa wababe hawa kusaka ushindi kutinga hatua ya nusu fainali.

1. Cape Verde vs Afrika Kusini
2. Mali vs Ivory Coast
3. Congo DR vs Guinea
4. Nigeria vs Angola.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad