MABINGWA wa Kombe la Azam Sports Federation, Yanga leo Januari 30 wanatarajiwa kushuka uwanja Azam Complex, kumenyana na Hausing FC.
Yanga ilitwaa taji hilo kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Azam FC fainali ilichezwa Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
Timu ya Yanga iligotea katika hatua ya robo fainali kwenye Mapinduzi 2024 ilipofungashiwa virago na APR FC ya Rwanda hivyo inakibarua cha kutetea taji hilo.
Ali Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga amesema kuwa kwenye mashindano yote ambayo wanashiriki malengo yao ni kutwaa mataji kutokana na uimara wa kikosi.
“Tuna kazi kubwa ya kufanya kwa ajili ya kupata matokeo kwenye mechi ambazo tunacheza, tunahitaji kutwaa mataji yote tuliyotwaa ikiwa ni ligi, Kombe la Shirikisho.
“Wachezaji wanatambua ushindani uliopo hivyo watapambana kwa ajili ya kupata matokeo mazuri kwenye mech ambazo tunacheza,” amesema Kamwe.
No comments:
Post a Comment