KOCHA SIMBA APIGA MKWARA HUU HAPA - Dizo Click

Dizo Click

Hot

Post Top Ad

Tuesday 30 January 2024

KOCHA SIMBA APIGA MKWARA HUU HAPA

 


KOCHA Mkuu wa Simba, Abdlehak Benchikha amesema kuwa kazi ni moja kwa wachezaji wake kusaka ushindi kwenye mechi ambazo watakuwa wanacheza.

Timu hiyo iligotea nafasi ya pili kwenye Mapinduzi 2024 iliposhuhudia mabingwa wakiwa Mlandege wakitwaa taji hilo mara ya pili mfululizo baada ya kuwanza 2023 walipowafunga Singida Fountain Gate.

Kwenye fainali ya Januari 13 iliyochezwa Uwanja wa Amaan baada ya dakika 90 ubao ulisoma Mlandege 1-0 Simba.

Benchikha ameweka wazi kuwa wamerejea kwenye mazoezi kwa ajili ya kupata ushindi kwenye mechi zao na wapo tayari kuendelea kuwa kwenye mwendo mzuri.

“Tumerejea kwenye mazoezi na kila kitu kinaendelea sawa.Ambacho kipo ni kuona kwamba tunakuwa kwenye kasi yetu nzuri kupata matokeo mazuri na kushinda.

“Ninapenda kuona tunaendelea kushinda ndio maana tupo kwenye uwanja wa mazoezi. Wachezaji wapo wengine wapya na wengine walikuwa hapa wakati uliopita tunaendelea kufanya nao kazi kwa ushirikiano mkubwa,” .

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad