SIKU NGUMU ZA YANGA ZINAGOTA MWISHO - Dizo Click

Dizo Click

Hot

Post Top Ad

Tuesday 30 January 2024

SIKU NGUMU ZA YANGA ZINAGOTA MWISHO

 


UNAWEZA kusema zilikuwa siku ngumu kwa mashabiki wote wa Yanga baada ya kukaa muda mrefu bila kuishuhudia timu yao ikicheza katika ardhi ya Tanzania, jambo ambalo linatarajiwa kugota ukingoni leo Januari 30.

Mabingwa hao watetezi watakakuwa na kibarua kusaka ushindi dhidi ya Hausing FC katika mchezo wa kombe la la Shirikisho la Azam Sports.

 

Mchezo huo unatarajiwa kufanyika katika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi jijini Dar ambapo utachezwa saa moja kamili usiku.


Yanga mara ya mwisho kucheza katika ardhi ya Tanzania ilikuwa ni Disemba 23, 2023 jambo ambalo linawafanya kuwa hawajacheza mechi yoyote tangia mwaka huu uanze.

 

Wananchi ambao mara ya mwisho kuiona Yanga ikicheza walikuwa ni Zanzibar katika michuano ya Mapinduzi Cup.

 

Katika mchezo huo wa mwisho kucheza ulikuwa ni mchezo wa ligi kuu dhidi ya Tabora United ambapo walifanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 liliofungwa na Clement Mzize huku asisti ikitolewa na Jesus Moloko ambaye kwa sasa sio mchezaji wa timu hiyo.

 

Katika hatua nyingine wananchi wamekaa siku 27 bila kuishuhudia timu yao ikiweza kucheza katika ardhi ya Tanzania hivyo leo itakuwa hivyo kwenye mchezo huo uaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

 

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad