NYOTA MPYA SIMBA APEWA ONYO MAPEMA - Dizo Click

Dizo Click

Hot

Post Top Ad

Tuesday 30 January 2024

NYOTA MPYA SIMBA APEWA ONYO MAPEMA

 


INGIZO jipya ndani ya kikosi cha Simba, Ladack Chasambi ambaye ni kiungo mshambuliaji amepewa onyo mapema kutofikiria atafanya makubwa ndani ya timu hiyo kwa kuwa bado anahitaji muda zaidi.

Chasambi kasajiliwa Simba akitokea Mtibw Sugar ya Morogoro alipokuwa ni chaguo la kwanza chini ya Kocha Mkuu, Zuber Katwila.
Shiza Kichuya nyota anayetumia zaidi ya mguu wa kushoto amesema kuwa ni muhimu kwa Chasambi kuwa makini na kujifunza zaidi baada ya kupata changamoto mpya.

Ikumbukwe kwamba Kichuya aliwahi kucheza ndani ya kikosi cha Simba hivyo anaitambua vema timu hiyo yenye maskani yake Msimbazi, Kariakoo.

"Namtambua Chasambi ni mchezaji mzuri na amepata nafasi ya kujiunga na Simba ambayo ni timu kubwa. Anahitaji muda ili kufanya vizuri asifikirie kwa wakati huu anaweza kufanya makubwa bado atajiongezea presha kubwa ikiwa ataanza kuwaz hivyo,".
Simba kwa sasa ipo kwenye maandalizi ya mchezo wa raundi ya pili dhidi ya Tembo FC mchezo unaotarajiwa kuchezwa Januari 31, Uwanja wa Azam Complex. saa 1:00 usiku.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad