KUTOKANA na kitendo chake cha kupoteza muda mwamuzi wa kati Nassoro Mwinchui aliweza kumuonyesha kadi ya njano kipa Shaban Kado.
Mbali na kadi hiyo aliweza kutimiza majukumu yake vema akiwa na jezi ya Mtibwa Sugar wakati wakiibana Simba kushindwa kupenya katika ngome za Mtibwa Sugar, Uwanja wa Manungu.
Kado alikuwa ni mchezaji bora wa mchezo wakati wakigawana pointi mojamoja kutokana na umakini wake wa kuokoa hatari.
Ilikuwa ni dakika ya 18,31,36,39,47 na 76 aliwez kufanya yake na hatari kubwa ilikuwa ni ile ambayo aliifanya Abdi Banda wakati wa kuokoa ila Kado aliweza kusepa nayo.
No comments:
Post a Comment