SIMBA imepoteza mbele ya RS Berkane kwa kufungwa mabao 2-0 ikiwa ugenini mchezo wa Kombe la Shirikisho hatua ya makundi ikiwa ni kundi D.
Ulikuwa ni mchezo ambao RS Berkane walitawala kila eneo na kupata ushindi huo ambao unawafanya wawe vinara wa Kundi D.
Maumivu kwa wawakilishi wa Tanzania yalipelekwa na Adama Ba dk 32 na Charki El Bahri dk 41 na RS Berkane walipiga mashutu 19 na matano yalilenga lango.
Simba haikuwa bora upande wa ushambuliaji ilipiga mashuti mawili ambayo hayakulenga lango na ilifanya umiliki wa asilimia 35 huku RS Berkane walkwa na asilimia 65.
No comments:
Post a Comment