CHELSEA YAWEKWA SOKONI - Dizo Click

Dizo Click

Hot

Post Top Ad

Thursday, 3 March 2022

CHELSEA YAWEKWA SOKONI




ROMAN Abramovich usiku wa Jumatano kwa hisia amethibitisha kwamba yupo kwenye mpango wa kuiuza timu hiyo.


Abramovich ameamua kuuvunja ukimya baada ya taarifa kuwa nyingi zikieeleza kwamba tayari timu hiyo ipo sokoni.


MailOnline mapema Jumatano iliripoti kwamba Chelsea imewekwa sokoni na kiasi ambacho kilikuwa kinahitajika ni Euro bilioni 3.


Abramovich usiku uliopita amesema:"Nimeamua kuchukua maamuzi kuhusu timu ambayo ninaipenda kutoka ndani ya moyo wangu.


"Kwa hali ilivyo,nimeamua kuchukua maamuzi ya kuiuza timu....sitauliza kuhusu habari za madeni kulipwa,".


Abramovich ameielekeza benki ya  Marekani kusimamia shughuli nzima za mauzo ya timu hiyo.


Bilionea wa Usiswi, Hansjorg Wyss anatajwa kuweza kuinunua timu hiyo ambapo anahitaji wawepo wawekezaji wengine sita au saba.


Sababu zinazotajwa kuweza kuiweka sokoni Klabu ya Chelsea pamoja na raslimali nyingine za bilionea huyo ni kile kinachoendelea ndani ya Urusi akidaiwa kuwa na urafiki na rais wa nchini humo Vladimir Putin ambaye ameanzisha vita na Ukraine.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad