Simba SC vs Nsingizini Hotspurs CAF Champions, kitaumana kwa Mkapa kwa wababe hawa Oktba 26 kila timu kusaka tiketi ya kutinga hatua ya makundi.
Ikumbukwe kwamba katika mchezo wa kwanza ugenini
Oktoba 19,2025 ilikuwa Nsingizini Hotspurs 0-3 Simba SC. Mchezo wa maamuzi
utapigwa Uwanja wa Mkapa kwa wababe hawa wawili kusaka timu itakayokwenda hatua
ya makundi.
Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na
Mawasiliano Simba SC ameweka wazi kuwa huo ni mchezo wa kazi na watapambana
kupata matokeo mazuri uwanjani.
“Kikosi Jumatano kinarudi Mo Simba Arena
kuanza maandalizi ya mchezo wa Jumapili. Tunayo furaha ya kocha wetu Seleman
Matola amemaliza adhabu yake hivyo atakuwepo kwenye benchi Jumapili kuendelea
na majukumu yake.
“Kuelekea mchezo huu tumeweka viingilio vya
kitajiri. Viingilio ni Tanzanite - Tsh. 250,000, Platinum - Tsh. 150,000, VIP A
- Tsh. 30,000, VIP B - Tsh. 20,000, VIP C - Tsh. 10,000 na Mzunguko - Tsh.
5,000.
“Afrika hii timu zenye uhakika wa kucheza
makundi mara saba mfululizo ni Al Ahly na Mamelodi na sisi tunaongezeka hapo.
Ni mechi ambayo inatuongezea thamani kwenye klabu yetu. Na Mwanasimba asitokee
akaidharau hii mechi, tuutizame huu mchezo kama mchezo mpya. Itakuwa haina
maana yoyote tuje hapa tufungwe bao moja au mbili au twende matuta hatupo
tayari kuona hiyo fedheha. Tuhesabu bado ni bilabila.
“Mpaka sasa sisi tumeshinda mechi moja na bado
hatujafuzu. Mechi hii ya kufuzu tunataka kujaza uwanja wa Mkapa, hatutakiwi
kuchukulia poa, kwenye mpira hakuna kitu cha kawaida. Twendeni tukaujaze Uwanja
wa Benjamini Mkapa. Na sare yetu siku ya Jumapili itakuwa ni jezi nyekundu ya
kuscan. Usije na jezi ya zamani tafadhali, kila Mwanasimba aje na jezi mpya ya
Jayrutty.
“Wanasimba tunasababu za kuja uwanjani maana
mechi iliyopita tuliangalizia mchezo tukiwa Coco Beach, ilituuma. Tunalazimika
kwenda uwanjani ili kumkaribisha Meneja Dimitar Pantev akutane na Wanasimba kwa
mara ya kwanza, aione Simba Sports Club ipoje. Kwa kifupi Oktoba 26 itakuwa
Simba Day ya Pantev maana ile nyingine hakuwepo," Semaji Ahmed Ally.
.jpg)


.jpg)

.jpg)
